Wednesday, 15 January 2014

Viatuzi

Kiatuzi hiki kinafaa sana kwa kuvalia skirt , kigauni au hata trouser , na ninachokipendea zaidi ni kwamba unaweza kukivaa kazini au hata kwenye mitoko flani ambayo ungependa uonekane simple . 

Ni muhimu kwa kila mwanamke hasa kama unaweza viatu virefu kuwa na pair moja au hata tatu za viatu ponted vyeusi , kwani viatuzi hizi hufanya uonekane smart na kukufanya unekani maridadi zaidi . Mambo mazuri kama haya yanapatikana Viatuzi kwa bei poa kabisa karibuni .

Round toes na mid high heel , ni kiatu ambacho kitakufanya uwe very comfortable hasa kama mguu wako nii menene au widefit ,na kiatu hiki unaweza ukakivaa siku nzima ukiwa ofisini kwako , wala hautakuwa na haja ya kuvaa zile sandals ambazo tunaficha chini ya meza zetu.

Block heel  shoes  ni nzuri sana kwa wale ambao wanaoenda viatuzi virefu lakini hawawezi visigino vyembamba . kiatu hiki kinafaa sana kuvaliwa kazini na unaweza ukakivaa na skirt au hata suruali.

Red satin peep toes , kiatuzi hiki kinafaa sana kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile harusi , kitchen party au mtoko flani wa jioni .  Ni muhimu kwa mwanamke wa kileo kuwa na hata pair moja ya kiatu chekundu ,kwani kama ilivyo kwa kiatu cheusi kiatu chekundu pia huendana na nguo nyingi . 

Orange leather wedge , waswahili tuna msemo unaosema kizuri chajiuza , nadhani hapa kwenye hii wedge ya orange wala sina haja ya kuongea sana maana juu kimetegenezwa na ngozi na huku chini ni mbao , hapa ushindwe wewe tu maana ukikinunua utakivaa mpaka upate value for money . 

Round Toe sling back , kiatuzi hiki ni kirefu kiasi , lakini kiko very comfortable , yaani unaweza hata ukakimbia nacho , mbali ya kuwa mimi ni mtu wa mizunguko mingi , kiatu hiki nimekivaa na kuzunguka nacho mjini tena kwa muda mrefu bila tatizo lolote, na mbali ya hayo yote kwa kweli kinapendeza sana miguuni  , and hivi ndio vile tunaviita multi purpose maana kazini unakivaa , kanisani , au hata kwenye mitoko yako mbalimbali.

Golden Chain wedge , I love this pair . Mimi si mpenzii sana wa wedges lakini hiki kimenikosha , maana ukivaa na kiwalozi chako ukatoka ,nina uhakika kila mtu atakuwa anautizama mguu wako na jinsi utakavyokuwa umepemdeza . Ungoja nini? wahi Viatuzi sasa ujipatie kiatuzi hiki.

Magongo , hii inanikumbusha enzi , tena siku zile  nikiwa mdogo , mama alikuwa anazo zake , nikiwa kama mtoto kilz alipokuwa navua , nilizivaa na kutemmbea nazo nyumba nzima . Kiatu hiki kinafaa sana weekend 


No comments:

Post a Comment

New arrivals

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...