Saturday, 15 October 2011
MIAKA MITANO YA 8020 FASHIONS NITOKE VIPI???
TAREHE 30/10/11 ,Saa tano mchana Takribani siku 14 tu yaani wiki mbili , Ukumbi wa diamond patakuwa hapatoshi , kwani siku hiyo , dada yetu , rafiki yetu na mjasiriamali mwenzetu atakuwa anasherekea miaka mitano tangu aanzishe blog yake. Hii ni nafasi nzuri sana kwa wadada wooote wale wajasiriamali na wale ambao labda hapo baadae wangependa kuwa wajasiriamali kukutana na kubadilishana mawazo , kuelimishana n.k
Siku yenyewe mambo ni ya kiafrica tuuuu, mambo ya back 2 Africa , hivyo hapo ni khanga na vitenge kwa kwenda mbele au hata kama ni vya kizungu basi shurti uweke uasilia . Mie bado nawaza nitoke vipi , sijui nivae moja ya nguo nimevaa kwenye kitchen party ??? au Nimtafute CHICHIA anifanyie mambo.......
Viatuzi kama kawaida yetu tutakuletea viatuzi na viambatanisho vya kufa mtu , kama unavyoona hao models hapo mambo ya viatuzi na viambatanisho ni kutoka kwetu , nguo ni za CHICHIA designer wa kibongo ambae yuko london lakini nguo zake zinapatika hapa hapa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
New arrivals









No comments:
Post a Comment