Friday, 20 January 2012

THANK YOU FOR YOUR SUPPORT

Leo Viatuzi inafikisha miaka miwili tangu ifunguliwe , napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru MWENYEZI MUNGU,  kwa neema na baraka tele anazoendelea kutupa , WAZAZI  WANGU  kwa msaada mawazo mazuri wanayonipa , DADA na KAKA zangu kwani bila ndugu zangu Viatuzi isingekuwa hapa ilipo . Pia  marafiki ambao wameshakuwa   madada na makaka  zangu , siwezi kuwataja mmoja moja ,ila ninachoweza kusema ni asanteni sana. SHAMIM Zeze A.K.A 8020 fashions asante  kwa support uliyotupa tangu tumeanza mpaka hivi leo na unayoendelea kutupa  , TEDDY KAEGELE asante kwa blog yako imekuwa msaada mkubwa sana kwetu. Na mwisho kabisa napenda kuwashukuru SHOE LOVERS WOTE , siwezi kuwataja mmoja mmoja but kutoka moyoni mwangu nasema asanteni sana kwa kuwa pamoja nasi na kutushika mkono kwa support yenu na upendo wenu.  Viatuzi tunawaahidi mambo mazuri saaaana mwaka huu , na maoni yenu ninayafanyia kazi  , Mungu awabariki sana na Asanteni.

Olivia 
Viatuzi





1 comment:

New arrivals

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...