Friday 20 January 2012

Takribani miaka mitatu iliyopita nilianza , kuuza Viatuzi , lakini kama mjasiriamali yoyote mdogo , nilianzia  taratibu na sibuwa na duka bali niliuzia mzigo wangu kwenye sebuleni  , na kwenye gari yaani I was also selling shoes from the boot of my car . Tuliotoka nao mbali wanakumbuka  na baada ya mwaka mmoja wa kuanza na kuuza bidhaa mkononi Baba na Mama yangu wakaniwezesha , ili niweze kupata sehemu ya kuuzia badala ya kuuzia sebuleni , Pale home palikuwa na parking ambayo siku za nyuma Mama alijenga kibanda ambacho kilitumika kama salon ya wanawake ya nywele n.k Wazee hao wakaona wanipe hicho kisehemu ili nipatengeneze , na nifanyie shughuli zangu humo . Basi matengenezo yakaanza kama unavyoona hapo chini kwenye pichazi.





Ilipofika tarehe 21/01/2010 matenngenzo yakawa tayari na tukafungua  na ndugu , jamaa na marafiki wa karibu.















No comments:

Post a Comment

New arrivals

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...